Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Agizo la RC DSM "Mwananchi akikataa kuvaa Barakoa asipande gari/Ni Amri"

Video Archive
Tue, 3 Aug 2021 Chanzo: millardayo.com

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa tamko la Kusisitiza matumizi sahihi ya Barakoa kwa kila abiria wote wanaopanda kwenye Vyombo vya Usafiri huku akiwataka Wamiliki wa Vyombo hivyo kuwaelekeza Madereva na Makondakta kuepuka kubeba abiria asievaa Barakoa.

RC Makalla ametoa msisitizo huo wakati wa kikao Cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kilichoketi kupitia tathimini ya utekelezaji wa mwongozo uliotolewa na Wizara ya Afya juu ya kujikinga na Corona na kuendelea kusitiza Suala la level seat.

Mh Makalla amesema kumekuwa na ulegevu wa usimamizi kwenye baadhi ya maeneo ambapo ametoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Wilaya na LATRA kuhakikisha wanasimamia ipasavyo mwongozo wa Wizara ya Afya.

Kutokana na changamoto za usafiri kwa wanafunzi, RC Makalla ameruhusu Daladala kubeba Wanafunzi watano watakaosimama lakini kwa kigezo Cha Wanafunzi hao kuwa wamevaa Barakoa.

Chanzo: millardayo.com