Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Agizo la Makonda kwa watendaji wa mitaa Dar

73396 Makondapic

Thu, 29 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amewataka watendaji wa mitaa kuhuisha daftari la wakazi wa maeneo yao ili kuwatambua na kujua shughuli wanazofanya.

Amesema wasipofanya hivyo ni rahisi kujipenyeza watu wasio na nia njema na kusababisha vurugu hasa kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa Serikali za mitaa na uchaguzi mkuu.

Makonda ametoa kauli hiyo leo Alhamisi Agosti 29, 2019 wakati akizindua mkakati wa kudhibiti wahamiaji haramu katika Mkoa huo.

Amesema ni wajibu wa watendaji wa mtaa kuweka utaratibu wa kuwatambua wakazi wao ili ikitokea tatizo iwe ni rahisi mhalifu  kujulikana.

Akizungumzia mkakati huo, Makonda amesema utasaidia kujenga mahusiano bora zaidi kuhakikisha mkoa unakuwa salama.

“Nawasihi watendaji  watakaopata mafunzo kuzingatia sheria,  taratibu na kanuni. Hatutapenda mkakati huu ukaingia doa kwa watu wasiokuwa na hatia kutengenezewa hatia ili wachache wanaopenda rushwa  wajichukulie fedha,” amesema.

Pia Soma

Ofisa uhamiaji Mkoa wa Dar es Salaam, kamishna msaidizi, Novaita Mrosso amesema lengo la mkakati huo ni kuanzisha mfumo wa udhibiti wa uhamiaji haramu.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz