Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Agape watoa kifaa maji tiririka shuleni

Agapeeee Ed.webp Agape watoa kifaa maji tiririka shuleni

Tue, 16 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirika lisilo la kiserikali la Agape linalotetea haki za watoto mkoani Shinyanga, limetoa kifaa cha kisasa cha majitiririka katika shule ya msingi Lubaga iliyopo mjini Shinyanga, kwa ajili ya wanafunzi kunawa mikono ili kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizo ya virusi vya Corona

Shirika lisilo la kiserikali la Agape linalotetea haki za watoto mkoani Shinyanga, limetoa kifaa cha kisasa cha majitiririka katika shule ya msingi Lubaga iliyopo mjini Shinyanga, kwa ajili ya wanafunzi kunawa mikono ili kuendelea kuchukua tahadhari ya kujikinga na maambukizo ya virusi vya Corona.

Akizungumza leo wakati wa kukabidhi kifaa hicho Mkurugenzi wa Shirika hilo, John Myola amesema wametoa kifaa hicho kama sehemu ya kuadhimisha siku ya mtoto wa afrika, ambapo pia Rais John Magufuli ameshatangaza kuwa shule zifunguliwe juni 29 mwaka huu, ndipo wakaona ni vyema kuendelea kuwalinda wanafunzi dhidi ya Corona.

Amesema shirika hilo la Agape linashughulika na masuala ya utetezi wa haki za watoto, ndio maana wameguswa na kuanza kutoa vifaa vya kisasa mashuleni kwa ajili ya wanafunzi kunawa mikono kwa sabuni na majitiririka, ili wawe salama wakati wakiendelea na masomo yao.

“Leo ni siku ya maadhimisho ya mtoto wa afrika, ambapo sisi kama shirika la Agape tukaona tuadhimishe kwa kutoa kifaa cha kisasa cha majitiririka katika shule hii ya Msingi Lubaga, ili june 29 wanafunzi watakapofungua shule, waanze kukitumia na kuendelea kujikinga na maambukizo ya virusi vya Corona,” amesema Myola.

“Naomba pia wadau ambao wanashughulika na masuala ya utetezi wa haki za watoto, walione suala hili kwa mapana na kwenda kutoa misaada ya vifaa hivi vya majitirika mashuleni, ili kuendelea kuwalinda watoto dhidi ya maambukizo haya ya virusi vya Corona,”ameongeza.

Naye Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Stella Lucas, amelipongeza Shirika hilo la Agape kwa kutoa msaada huo wa kifaa cha majitiririka, huku akiomba wadau wengine wajitokeze kuwasaidia, ambapo bado wanauhitaji mkubwa huku shule hiyo ikiwa haina fedha za kutosha kununua vifaa hivyo.

Kwa upande wake mtendaji wa Kata ya Lubaga Lucas Venance, ameliomba shirika hilo kuendelea kuchangia vifaa hivyo cha kujikinga na maambukizo ya virusi vya Corona mashuleni pamoja na wadau wengine, ikiwa Kata hiyo ina shule mbili za msingi Lubaga na Azimio ambazo zote zinauhitaji mkubwa wa vifaa vya majitirika ili wanafunzi wajikinge na Corona.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live