Thu, 11 Nov 2021
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Mkuu wa mkoa wa Simiyu David Kafulila amemsimamisha kazi Afisa Ushirika wa Wilaya ya Maswa Joseph Dachi ili kupisha uchunguzi kutokana na tuhuma zinazomkabili za ubadhirifu wa fedha,
RC huyo ameitaka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kufanya uchunguzi dhidi yake na sheria ichukue mkondo wake .
Ameyasema hayo akiwa kwenye kikao cha Baraza la Madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Maswa na kuwasisitiza TAKUKURU kufanya uchunguzi wa kina ili kubaini njia zte zilizotumika kuiba fedha hizo, na kufahamu wale wote waliohusika na mpango huo dhalimu.
Chanzo: www.tanzaniaweb.live