Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afariki kwa kudondokewa na ukuta Moro

Kifo 00263246 Afariki kwa kudondokewa na ukuta Moro

Fri, 5 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtu mmoja Ibrahim Juma Ramadhan (44), amefariki baada ya kuangukiwa na ukuta wa ghorofa lililopo mtaa wa Sugume Kata ya Mwembesongo Manispaa ya Morogoro.

Kamanda wa Jeshi la zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Morogoro, Shaban Marugujo amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema walifanikiwa kumuokoa mtu mmoja aliyebanwa na ukuta sehemu za miguu yake akiwa hai lakini alifariki baadaye.

Amesema, sababu za ukuta huo kuanguka ni kutokana na jengo lililokuwa linajengwa, kujengwa chini ya kiwango, hali iliyopelekea sehemu ya ukuta kumeguka na kudondoka, huku akiwataka Wananchi kuchukua tahadhari katika maeneo yote ambayo ujenzi unaendelea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live