Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afariki baada ya kufunga siku 30, aliahidi atafufuka

Bible Verses 1 Afariki baada ya kufunga siku 30, aliahidi atafufuka

Thu, 15 Dec 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali isiyokuwa ya kawaida Mtu mmoja anayefahamika kwa Jina la Abdel Raphael (42) Mkazi wa Mtaa wa uwanja Wilaya ya Geita Mkoani Geita amekutwa amefariki kwa kile kinachodaiwa alifunga maombi ya sala kwa siku 30 katika chumba chake huku akiiaminisha Familia yake kuwa akifariki atafufuka baada ya siku nane.

Mmoja wa waumini waliokuwa wakishiriki katika Ibada hiyo ya kufunga na kuomba, Kanyasu John amekiri kuwepo kwa Ibada hizo zilizokuwa zikifanyika nyumbani kwake ambapo amesema Abdel aliwaaaminisha baada ya siku 30 za mfungo atafariki kisha atafufuka maana ameoteshwa.

"Tulijenga Hekalu tukatangaza kwa awamu ya kwanza ikawa imepita lakini kwa awamu hii tukatangaza mwezi wa 10 kufikia hii awamu ya mwezi wa 11 akasema ni wakati wa kwenda kutangaza neno akasema Mungu amemwambia wakati wa kwenda kutangaza Dini umefika kwahiyo atulete sisi kwenye Ibada ya muda mrefu wakati yeye akiendelea na Ibada nyingine kwahiyo sisi tukaingia kwenye maombi ya mwezi mzima kuanzia tarehe 8 mpaka tarehe 8”

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa wa Uwanja Ennos Cheleani amekiri kupokea taarifa hizo hali ambayo ilipelekea kufika eneo la tukio ili kujiridhisha ndipo waliposaidiana katika kuhakikisha Mwili wa Marehemu unafikishwa Hospitali kwa ajili ya uchunguzi .

Chanzo: www.tanzaniaweb.live