Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Afa akizungumza na simu iliyokuwa kwenye chaji

94630 Pic+simba Afa akizungumza na simu iliyokuwa kwenye chaji

Thu, 6 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Serengeti. Vumilia Kitang'enyi (19), mkazi wa Serengeti  amekufa wakati akizungumza na simu aliyokuwa ameichomeka kwenye chaji.

Taarifa zilizolifikia Mwananchi zinaeleza kuwa tukio hilo limetokea leo Jumatano Februari 5, 2020, kwamba  Vumilia alikutwa amekufa akiwa amepiga magoti huku ameshika simu mkono wa kushoto. Amekutwa na majeraha  ya kuungua katika shavu la kushoto.

Mganga mkuu wa hospitali ya Nyerere, Tanu Warioba amethibitisha kifo cha Vumilia lakini hakuwa tayari kueleza suala hilo kwa kina.

Akizungumza na Mwananchi mwenyekiti wa mtaa wa Sedeko eneo la Mugumu Mjini,  Charles Chacha amesema Samwel Joseph maarufu Wazo alimkuta Vumilia ambaye ni mkewe akiwa amepiga magoti huku mkononi akiwa ameshika simu.

Amesema simu hiyo ilikuwa katika chaji na alipomchunguza alibaini amebabuka katika shavu lake la kushoto.

"Soketi aliyochomeka chaji inaonekana ilikuwa mbovu, naye kwa kuwa alikuwa anafua alikuwa na majimaji  na katika sakafu kulikuwa na unyevunyevu kutokana na mvua zinazonyesha, inawezekana ni chanzo cha kifo chake," amesema Chacha.

Pia Soma

Advertisement
Mwenyekiti huyo wa Serikali ya mtaa amesema mafundi wa Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) walifika katika nyumba hiyo na kufanya ukaguzi ambapo walibaini  mfumo wa umeme katika nyumba hiyo una shida.

Byabato Wenchislaus, shuhuda wa  tukio hilo amesema ,” mumewe aliporudi alimkuta Vumilia ameanguka huku mkononi akiwa na simu ameing’ang’ania. Awali alidhani amepiga magoti na alipomtazama alibaini amekufa, alianza kupiga kelele ndio tukajitokeza kumsaidia.”

Amesema watu ambao Vumilia aliwaacha nje wakati akiingia ndani, walishangaa walipopata taarifa za kifo chake kwa kuwa hawakusikia hata akipiga kelele kuomba msaada.

Chanzo: mwananchi.co.tz