Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adha usafiri Ziwa Tanganyika kutatuliwa

Ziwa Tanganyikarr Adha usafiri Ziwa Tanganyika kutatuliwa

Tue, 10 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Komredi ameeleza hatua mbalimbali zinazochukuliwa na Serikali, kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya 2020 – 2025, kwa vitendo, kuboresha huduma za uchukuzi, usafiri na usafirishaji katika Ziwa Tanganyika, ambapo kufikia mwezi Disemba, 2023, wananchi wataanza kupata nafuu, kuelekea kumalizika kwa adha kubwa iliyopo sasa.

Unafuu huo utatokana na kukamilika kwa matengenezo ya moja ya meli, kati ya mbili zilizopo sasa, Mv Mwongozo na Mv Liemba, ambazo zote zinafanyiwa matengenezo, ikiwa ni mojawapo ya mikakati ya muda mfupi, wa kati na mrefu, pamoja na kutengeneza meli mpya, kwa ajili ya shughuli za kiuchumi na wananchi kwa ujumla, ambazo hatimae zitaondoa na kumaliza kabisa changamoto ya usafiri na usafirishaji katika maeneo ya mwambao wa Ziwa Tanganyika, kuunganisha hadi nchi jirani za DR Congo na Zambia.

Katibu Mkuu wa CCM, Komredi Chongolo ametangaza mikakati hiyo alipokuwa akizungumza na wananchi wa maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Kalambo, Jumatatu Oktoba 9, 2023, ambapo anaendelea na ziara yake katika Mkoa wa Rukwa, yenye malengo ya kuhamasisha uhai wa CCM, kusikiliza changamoto za wananchi na kuzitafutia ufumbuzi na kukagua utekelezaji wa Ilani ya CCM ya 2020 – 2025, kwa kutembelea miradi ya maendeleo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live