Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adakwa akiiba sadaka kanisani

KUTOA SADAKA Adakwa akiiba sadaka kanisani

Wed, 11 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Katika hali isiyo ya kawaida kijana mmoja amekamatwa akiiba sadaka katika viunga vya kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es Salaam.

Paroki wa kanisa hilo Alister Makubi amethibitisha kutoka kwa tukio hilo jioni ya jana Mei 10, ambapo kijana huyo alikamatwa na walinzi waliokuwa kanisani hapo.

“Ni kweli tukio hilo limetokea jana katika kanisa la kuabudu ekaristi ambapo huwa wanakuja watu mbalimbali kila mmoja akiwa na maombi yake kwa Mungu wake.

“Ila inaonekana huyu kijana alikuja na nia yake nyingine maana hadi ilipofika jioni alionekana katika eneo lile yupo peke yake, huenda walinzi walihisi kitu maana walipomfuatilia walimkuta anachota hela katika sehemu ambayo watu wanaweka sadaka,” amesema paroko huyo.

Video inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii inamuonyesha kijana huyo akihohiwa na walinzi baada ya kunaswa akiwa ameshika fedha hizo.

Katika mahojiano hayo alikiri kuiba sadaka na kueleza wazi kuwa si mara yake ya kwanza kufanya kitendo cha aina hiyo kanisani hapo.

Paroko Makubi amesema suala hilo lipo mikononi mwa jeshi la polisi na kampuni ya ulinzi inayolinda kanisani hapo ndiyo inalishughulikia.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live