Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kuwaua wanawake wawili kisha kujisalimisha polisi

PANGA Ed Adaiwa kuwaua wanawake wawili kisha kujisalimisha polisi

Sat, 7 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wanawake wawili wa familia moja, Steria Gabriel (73) na Paulina Mathias (51), wakazi wa Kijiji cha Nyaishozi Wilaya ya Karagwe wameuawa kwa kukatwa panga na mtu anayedaiwa kuwa ni mmoja wa wanafamilia.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, Blasius Chatanda amesema mauaji hayo yametokea Oktoba 5, 2023 na uchunguzi unaendelea kuwezesha mtuhumiwa (jina linahifadhiwa) kuchukuliwa hatua za kisheria.

‘’Ninachoweza kwa sasa ni kuthibitisha tukio hilo kutokea, siwezi kulizungumzia kwa undani kwa sababu nasubiri taarifa kutoka kwa maofisa wangu wilayani Karagwe,’’ amesema Kamanda Chatanda

Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nyaishozi, Salvatory Mtunzi ameiambia Mwananchi anayedaiwa kufanya mauaji haya alijisalimisha Kituo Kidogo cha cha Polisi Nyaishozi mara baada ya tukio hilo.

Amesema baada ya kushikiliwa kwa muda Kituo cha Nyaishozi, mtuhumiwa huyo alihamishiwa Kituo Kikuu cha Polisi Wilaya ya Karagwe mjini Kayanga.

Amesema kabla ya tukio la sasa, mtuhumiwa huyo pia amewahi kutuhumiwa, kushtakiwa na kuhukumiwa kifungo jela kwa mauaji ya mtoto wa jirani zake kwa kumponda mawe.

‘’Baada ya kumaliza kifungo na kutoka jela, alifukuzwa hapa kijijini na kuhamia Kijiji cha Bushangaro hadi jana alipoonekana hapa kijijini kabla ya kufanya mauaji,’’ amesema Mtunzi

Mmoja wa majirani aliyejitambulisha kwa jina la Alfred Christian aliviomba vyombo vya dola kufanya uchunguzi wa kina na kuchukua hatua stahiki kukomesha vitendo vya aina hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live