Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kumuua mkewe akimtuhumu kumuambukiza magonjwa ya zinaa

Maambukizipic Data Kaimu Kamanda wa Polisi mkoa wa Mtwara, Nicodemas Katembo

Sat, 2 Apr 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara limemkamata Shaibu Kuselela (58) anayedaiwa kumuua mkewe Amina Mtausi (40) na kumzika shambani kwa madai marehemu alimuambukiza magonjwa ya zinaa.

Akizungumza Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani humo, Nicodemas Katembo amesema katika mahojiano ya awali mtuhumiwa huyo amekiri kufanya mauaji hayo kwa kudai mkewe alimuambukiza magonjwa ya zinaa.

“Baada ya kupata taarifa hizo, tulianza ufuatiliaji kupitia taarifa fiche ili kumpata mtuhumiwa, taarifa hizi zilitusaidia na kufanikiwa kumkamata” amesema Kamanda Katembo.

Amesema mtuhumiwa alikamatwa Machi 25, 2022 katika kijiji cha Mvuleni, Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi ambapo amefikishwa katika mahakama ya Wilaya ya Tandahimba.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz