Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kujiua baada ya kumuua kaka, kumjeruhi mama yake

78286 Mauaji+pic

Thu, 3 Oct 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  William Lawi, mkazi wa mtaa wa Kinzudi-Majengo Salasala jijini Dar es Salaam amejiua baada ya kumuua kaka yake na kumjeruhi mama yake mkubwa.

William anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka kati ya 18 na 19 anadaiwa kutumia kisu na nyundo kumuua kaka yake,  Freddy Hamis na kumjeruhi mama yake mkubwa, Grace James.

Ndugu wa Lawi wamesema kabla ya kujinyonga, ndugu yao alikunywa sumu ya panya kwa kuwa walikuta mfuko wa sumu hiyo ukiwa umefunguliwa na kutumika.

Akizungumza na Mwananchi leo Alhamisi Oktoba 3, 2019 mjumbe wa mtaa huo,  Zabron Manyama amesema tukio hilo lilitoka usiku wa kuamkia Jumatatu Septemba 29, 2019.

Manyama amesema kabla ya kufanya mauaji, Theresia Halot ambaye ni bibi yake William alikwenda kumuona, akimtaka azungumze na kijana huyo kwa sababu alikuwa ameanza tabia ya wizi, kuvuta bangi.

"Walikuja na tukawa na kikao nilimuonya yule kijana kama mwanangu na bibi yake alimuonya kwa tabia hiyo. Ilikuwa Jumapili na saa tatu usiku kikao kiliisha," anasema.

Pia Soma

Advertisement
Manyama amesema kikao kilipoisha inadaiwa alianza kupita kwenye maduka kutafuta sumu ya panya na usiku alienda nyumbani kwa mama yake mkubwa.

"Alibisha hodi akafunguliwa na kaka yake akimwambia anataka kuongea na mama yake mkubwa, alipofunguliwa alimpiga na kumchoma kisu akaenda kwa mama yake na kumjeruhi pia," amesema Manyama.

Manyama amesema wakati tukio hilo likifanyika mtoto mwenye umri wa miaka tisa alikuwa akishuhudia alipotishiwa alikimbia kwenda kujificha.

Msemaji wa familia hiyo, Nchore Marwa amesema kijana huyo alipofika nyumbani baada ya kufanya mauaji alikunywa sumu na alipoona inamchelewesha akaamua kujinyonga kwa kutumia shuka.

Mwili wa Lawi utazikwa leo jijini Dar es Salaam.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz