Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Adaiwa kufariki kwa kuzidiwa na pombe

Kifo Kifo Mauiaji.png Adaiwa kufariki kwa kuzidiwa na pombe

Fri, 17 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kijana aitwaye Magoke Frances (31), Mkazi wa Mtaa wa Elimu Halmashauri ya Mji Geita amekutwa amefariki katika nyumba aliyokuwa akiishi ambapo Mpwa wa marehemu, George Charles amesema Ndugu yao alikuwa ni Mtumiaji sana wa pombe na amaamini ndio chanzo cha kifo chake.

"Marehemu alikuwa ni Mtu wa pombe sana, pombe ambazo ni za kienyeji hizi taarifa hizi nimezipata nikiwa Kasamwa baada ya kuuliza nikaambiwa kwamba yumo ndani amekufa ana siku tano sasa "

Hassan Malima ni Mwenyekiti wa Mtaa wa Elimu amekiri kupigiwa simu na Kamanda wa Polisi Jamii katika Mtaa huo ambaye alimpa taarifa za Mtu huyo kufia ndani ya nyumba, Malima amesema tukio kama hilo kujitokeza katika Mtaa wake ni la pili ambapo amewataka Vijana wenye umri mkubwa wanaoishi pekee yao waoe maana matukio yamekuwa yakihusiaishwa na ulegi kupindukia pamoja na msongo wa mawazo.

Akithibitisha kutokea kwa Tukio hilo Kaimu Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Geita Adamu Maro amesema uchunguzi wa awali wa Daktari unaonesha alikosa hewa wakati akiwa amelewa nyumbani kwake.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live