Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Achomwa moto hadi kufa madai ya wizi wa ng’ombe

Almachius Ed Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Almachius Muchunguzi.

Mon, 2 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Ramadhani Omari (24), mkazi wa mji wa Pongwe jijini Tanga, ameuawa kwa kuchomwa moto na wananchi wenye hasira, akidaiwa kushiriki kuiba ng'ombe na wenzake ambao walikimbia.

Tukio hilo lilitokea juzi alfajiri maeneo ya kijiji cha Tanganyika, Kata ya Lusanga nje kidogo ya mji wa Muheza huku wazazi wa kijana huyo, wakianguka na kupoteza fahamu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tanga, Almachius Muchunguzi, alisema baada ya wezi hao kuiba ng’ombe huyo kambi ya Kitisa kwa mfugaji Daud Raymond ( 48), walikwenda kumchinja katika mashamba yaliyoko katika kijiji cha Tanganyika wilayani hapa.

Alisema wakati wezi hao wakibeba nyama, ndipo kundi la wafugaji liliibuka alfajiri hiyo na kuanza kuwasaka baada ya kupeana taarifa kuhusu wizi huo.

Kamanda Muchunguzi alisema wafugaji hao wakati wanawasaka wezi hao waliwakuta kijijini hapo wamemchinja huku kukiwa na ushahidi wa kwato, utumbo na kichwa.

Alisema wezi hao baada ya kuwaona wafugaji, walikimbia na Omari ambaye ni marehemu, aliyekuwa na pikipiki yenye namba MC 907 DXR, alishindwa kukimbia ndipo alivamiwa na kupigwa hadi kufa na kuchomwa moto yeye na pikipiki yake.

Alisema, Omari aligundulika na wapita njia ambao walitoa taarifa polisi wilaya ya Muheza ambao walifika wakiongozwa na Mkuu wa Upelelezi Wilaya, Charles Ntenga, na kuchukua mwili ambao umehifadhiwa Hospitali Teule ya Muheza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live