Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Achomwa mkuki akifukuza mifugo shambani

Mkuki Wer.jpeg Achomwa mkuki akifukuza mifugo shambani

Mon, 27 Mar 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mohamed Salumu (44) mkazi wa Kijiji cha Olpopong kata ya Njoro wilayani Kiteto mkoani Manyara amenusurika kifo kwa kuchomwa mkuki kifuani wakati akizuia mifugo isiharibu mazao yake shambani.

Watuhumiwa hao waliamuru mifugo hiyo iharibu mazao hayo shambani ambapo jumla ya ekari 6 zimeteketezwa na mifugo hiyo.

Awali vijana hao walifika kwa mkulima huyo na kufungua uzio uliokuwa umewekwa hapo shambani na baada ya kuzuiwa mkulima huyo walimrushia mkuki ambao umemjeruhi kifuani na kwa sasa majeruhi huyo amelazwa hospitali ya wilaya ya Kiteto kwa matibabu zaidi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live