Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Achoma nyumba ya mpenzi wake kisa wivu wa Mapenzi

Nyumba Yachomwa Na Jose Achoma nyumba ya mpenzi wake kisa wivu wa Mapenzi

Fri, 10 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jeshi la Polisi mkoa wa Mwanza linamshikilia Joseph Hezron (54), mkazi wa Bukara wilayani Sengerema kwa kuchoma moto nyumba ya mpenzi wake aitwaye Lucy James, kisha kujaribu kujiua kwa kujichoma kisu shingoni huku chanzo kikitajwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Tukio hilo limetokea Novemba 9, 2023 katika mtaa wa Bukara baada ya Joseph kumtuhumu mpenzi wake huyo kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine aitwaye Jelemia Kamambi, ndipo alichoma nyumba hiyo na kupelekea hasara.

Uchunguzi uliofanywa na Jeshi la Polisi umebaini kuwa mwanaume ambaye Joseph alikuwa anamtuhumu hakuwa mpenzi wa mwanamke huyo (Lucy Hezron) bali alikuwa kaka yake, hivyo kuwataka wanaume kuacha wivu wa mapenzi uliopitiliza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live