Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abiria wanusurika kuteketea kwa moto ndani ya daladala Dar

69919 Pic+daladala

Mon, 5 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Daladala inayosafisha abiria kutoka Gongo la mboto kwenda Ubungo-Mawasiliano, Dar es Salaam nchini Tanzania imenusurika kuteketea baada ya injini yake kuwaka moto.

Ajali hiyo imetokea leo Jumatatu asubuhi Agosti 5, 2019 katika eneo la Tabata-Mwananchi wakati daladala hiyo yenye namba za usajili T658 DEB ilipokuwa inatokea Gongo la Mboto kwenda Ubungo huku ikiwa na abiria.

Mwananchi imeshuhudia abiria wakishuka ndani ya daladala hiyo yenye milango miwili huku wakikimbia ili kujiokoa na moto huo.

Wakizungumza na Mwananchi baadhi ya abiria wamesema tangu wakiwa kituo cha TOT (kituo kimoja nyuma kabla ya Mwananchi) walihisi harufu ya moto lakini walipomueleza dereva na kondakta kuhusu harufu hiyo hawakutilia maanani.

 “Tulipofika hapa Mwananchi ndio moshi ulizidi na ukawa umetanda gari zima hapo  ikabidi wasimamishe daladala ili tushuke, kibaya zaidi walikuwa na vifaa duni vya kuzimia moto,” amesema Asha Athman, mmoja wa abiria.

Kamanda wa Kikosi cha Zima moto kutoka kampuni ya SGA kupitia gari linalopaki kituo cha Mwananchi, Edwin Charles amesema walipobaini moto huo waliwasiliana na makao makuu haraka kabla ya kwenda kuuzima.

Pia Soma

“Tusingekuwepo hali ilikuwa mbaya kwa sababu hawakuwa na kifaa cha kuzimia moto chenye ubora, hivyo tumefanikiwa kuudhibiti,” amesema Charles.

Mtaalamu wa kuzima moto kutoka kikosi cha SGA, Enock Charles amesema madereva wanapaswa kuhakikisha magari wanayoendesha yanavifaa vya kuzimia moto vyenye uwezo badala ya vile vya kijanja wanavyohifadhi kuwakwepa polisi.

“Kama wangekuwa eneo lisilo na watu hali isingekuwa kama ilivyo kwa hiyo suala la kuwa na vifaa vya kuzimia moto sio kwa ajili ya kuwakimbia polisi isipokuwa uokozi,” anasisitiza.

Baadhi ya mashuhuda wamesema tangu wanaliona gari hilo kituo kimoja kabla halijapata hitilafu kulikuwa na moshi ambao ulipaswa kudhibitiwa mapema.

Kondakta wa daladala hilo ambaye hakutaka kutaja jina lake amesema japo hawakuweza kudhibiti moto huo lakini walikuwa na vifaa.

Chanzo: mwananchi.co.tz