Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abiria wanavyosotea usafiri Ubungo

33048 UBUNGO+PIC Tanzania Web Photo

Sun, 23 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Abiria wanaosafiri  kwenda mikoa mbalimbali wako njia panda na wengine wameamua kurudi nyumbani kutokana na kuadimika kwa usafiri katika Kituo Kikuu cha Mabasi Ubungo jijini Dar es Salaam.

Mwananchi lilifika kituoni hapo alfajiri ya leo Jumapili Desemba 23, 2018. Limeshuhudia umati mkubwa wa abiria wakihaha huku na huko kutafuta usafiri huku baadhi ya abiria wakilalamika kwamba walihakikishia adha hiyo.

Happiness Samson amesema toka saa 11 alfajiri amefika kituoni lakini hakuna tiketi wala gari lolote linalokwenda Mikumi mkoani Morogoro.

"Tulisikia kupitia vyombo vya habari kuwa hakutakuwa na shida ya usafiri lakini toka saa 11 nimefika hapa hakuna gari lolote," amesema Happiness.

Moses Mwenda anayekwenda Lushoto mkoani Tanga amesema jana Jumamosi alifika kituoni hapo kwaajili ya kukata tiketi lakini hakupata na leo toka saa  9 usiku hajapata gari wala tiketi.

"Toka saa 9 niko hapa sijapata usafiri baada ya jana kukosa tiketi na kuwaambiwa tuje leo lakini hali ni ileile," amesema Moses.

Abiria mwingine Anna Mboya amesema toka saa 10 amefika na watoto akitegemea atapata gari lakini ameshangazwa hata hayo binafsi yaliyopewa vibali hayapo.

Mkurugenzi wa usafiri na udhibiti wa barabara, Johansen Kahatano amesema wanaendelea kuhimiza watu wenye mabasi madogo kwenda kupewa vibali kwaajili ya kutatua changamoto hiyo.

"Abiria ni wengi sana huwa wanasafiri siku za mwisho pamoja na kutoa vibali vingi bado tunahimiza wenye mabasi madogo waje kuchukua vibali kwaajili ya kutoa huduma," amesema Kahatano.

 



Chanzo: mwananchi.co.tz