Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, ACP Safia Jongo, amewakemea baadhi ya abiria wanaohamasisha na kushabikia mwendokasi na madereva wanaokiuka sheria za barabarani, vitendo ambavyo vimekuwa vikisababisha ajali za mara kwa mara na kupoteza maisha ya watanzania huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Geita, ACP Safia Jongo, amewakemea baadhi ya abiria wanaohamasisha na kushabikia mwendokasi na madereva wanaokiuka sheria za barabarani, vitendo ambavyo vimekuwa vikisababisha ajali za mara kwa mara na kupoteza maisha ya watanzania huku wengine wakiachwa na ulemavu wa kudumu. Kamanda Jongo ameyasema hayo wakati akizungumza na madereva na abiria katika stendi kuu ya mabasi ya Mkoa huo katika uzinduzi wa Wiki ya Usalama Barabarani.