Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abiria wadai kulishwa biskuti zenye dawa za kulevya ndani ya basi, walazwa hospitalini

86179 Pic+abiria Abiria wadai kulishwa biskuti zenye dawa za kulevya ndani ya basi, walazwa hospitalini

Thu, 28 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Lindi. Abiria wawili waliokuwa wakisafiri na basi la Buti la Zungu kutoka Dar es Salaam kwenda Mtwara nchini Tanzania wamenusurika kifo baada kula biskuti zinazodaiwa kuwa na dawa za kulevya wakiwa ndani ya basi hilo.

Abiria hao ni Dadi Rashid (49) ambaye ni ofisa elimu taaluma Utete wilaya ya Rufiji mkoa wa Pwani na Omary Burian (27) mfanyakazi wa bodi ya korosho Dar es Salaam.

Akizungumzia tukio hilo leo Jumatano Novemba 27, 2019 Kaimu mganga mfawidhi Hospitali ya Sokoine mkoani Lindi, Idrisa Chande amethibitisha kuwapokea wagonjwa hao jana usiku Jumanne wakiwa hawajitambui na kwamba wanaendelea na matibabu hospitalini hapo.

Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi, Poudence Proteus amesema  amepokea taarifa hiyo  na atalizungumzia baada ya uchunguzi kukamilika leo Jumatano.

Chanzo: mwananchi.co.tz