Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Abiria wa MV Kazi watajwa wizi wa maboya

Mv Kaziii2 05 At 12.jpeg Abiria wa MV Kazi watajwa wizi wa maboya

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Meneja wa vivuko Kanda ya Mashariki na Kusini Mhandisi Lukombe King’ombe ametoa onyo kwa wezi ambao ni abiria wasio waaminifu wanaotumia kivuko cha MV. KIGAMBONI na MV. KAZI kuacha mara moja tabia ya wizi wa maboya ya kujiokolea kwani wizi huo unasababisha kupungua kwa maboya hayo na hivyo

kuhatarisha usalama wao pamoja na mali zao endapo itatokea dharura ya ajali wakati vivuko hivyo vinatoa huduma.

Mhandisi King’ombe ametoa onyo hilo leo Machi 10, 2024, wakati wa zoezi maalumu la kukagua na kuhesabu idadi ya vifaa vya kujiokolea vilivyomo ndani ya vivuko vinavyotoa huduma katika eneo hilo la Magogoni Kigamboni.

Imegundulika kuwa, baadhi ya abiria wasio waaminifu, wamekuwa na tabia ya kuiba vifaa hivyo hasa maboya ya kujiokolea ya kuvaa (life jackets) ambayo ndiyo yanaonekana kuwa rahisi kubebeka bila kuonekana kwa urahisi wakati wa kushuka kutoka katika vivuko hivyo.

Wizi huo wa maboya ya kujiokolea umeonekana kushamiri na hata wakati mwingine kusababisha vivuko kusimamishwa kutoa huduma na Mamlaka husika za Usalama ikiwemo Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania (TASAC) kutokana na kutokidhi vigezo vya usalama.

Mhandisi King’ombe ameongeza kuwa tabia hiyo ya wizi wa maboya ya kujiokolea imekuwa ikiingiza Serikali kwenye hasara kubwa kwakuwa inailazimisha itoe fedha nyingine mara kwa mara kwa ajili ya kugharamia ununuzi wa maboya mapya ili kukidhi matakwa ya kisheria ya uendeshaji wa vivuko pamoja na kuendelea kulinda uhai pamoja na usalama wa abiria na mali zao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live