Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ATCL kuanza kutua Kisongo, Arusha

E57bc046ed94bb3afc304271b90be918 ATCL kuanza kutua Kisongo, Arusha

Wed, 20 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

Katika kuhakikisha idadi ya watalii inaongezeka katika vivutio vya mbuga za wanyama kanda ya kaskazini, Kampuni la Ndege la Tanzania Air Tanzania (ATCL) imerejesha safari zake rasmi za Arusha kupitia Kiwanja cha ndege cha Kisongo ikiwa na lengo ya kusogeza huduma karibu kwa wateja.

Akizungumza wakati wa hafla ya kupokea ndege hiyo katika kiwanja cha ndege wa Arusha, Meneja wa ATCL Kanda ya kaskazini, Estermary Karumbo alisema kuwa kwa muda mrefu walisitisha huduma kupitia kiwanja hicho kutokana na changamoto mbalimbali ila kwa sasa wamerudi rasmi.

Alisema kuwa uwepo wa safari hiyo utasaidia kukuza utalii na kuweza kurahisisha huduma ya usafiri

Naye Meneja wa Kiwanja cha ndege cha Kisongo Arusha, Elipid Tesha aliwashukuru ATCL kurudisha huduma zake katika uwanja huo kwa kuwa itatoa fursa kutangaza utalii.

Chanzo: habarileo.co.tz