Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ALAT yawasha taa ya hatari Temeke, yataka tathimini matumizi ya fedha

Temeke Kujitathimini ALAT yawasha taa ya hatari Temeke, yataka tathimini matumizi ya fedha

Sat, 11 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumuya ya Tawala za mikoa Tanzania (ALAT) imeiomba Halmshauri ya Temeke kufanya tafiti juu ya fedha zinazotolewa kama inafaa katika utekelezajii ili kubaini kama inatekelezwa katika mfumo wa uratibu wa fedha za mikopo.

Akizungumza hayo Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Murshid Ngeze walipotembelea mradi wa Ujenzi wa madarasa saba katika shule ya Sekondari ya Migulani, na mradi wa uzoaji taka kutoka kwa kikundi cha kinamama yote iliyoko katika kata Migulani, amesema upo umuhimu wa kuanzisha mfumo wa mahesabu wa kudhibiti mikopo ya asilimia 10 ambayo imekuwa ikitolewa na halmashauri mbalimbali.

Ngeze amesema Serikali kuu imekuwa ikipeleka fedha katika Serikali za Mitaa, kwamba baadhi ya Serikali hizo zimekuwa hazifanyi vizuri ikiwamo kuzitumia fedha hizo ndivyo sivyo hivyo kwa kupitia ziara hiyo wajumbe wa ALAT wameona kuna umuhimu wa kutembelea miradi katika halmshauri ya Temeke na wameridhishwa na utekelezaji wake.

"Mifumo ipo na kompyuta zimekuja kurahisisha kazi zetu ndio maana ya tehema na Rais amekuwa akituambia kuwa tutumie teknolojia hiyo kurahisisha kazi na kuingiza fedha suala hili kama ALAT tunalichukua na tutatafuta wataalamu waweze kutengenezwa mfumo huu na badae tutaupeleka Serikalini ili waweze kuona kama unafaa kusaidia halmshauri Kudhibiti mikopo ya asilimia 10"alisema Ngeze.

Kwa upande wake Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu Wilaya ya Temeke, Charles Mkwidu amesema.Jumuiya ya ALAT imekuwa na mchango mkubwa katika kuhakikisha utekelezaji wa miradi kama ulivyokwenda ikizingatia Jumuiya hii inaundwa na wajumbe wa Halmashauri zote nchini.

Amesema Halmshauri hiyo ilipokea jumla ya fedha Sh 3.14 bilioni ambapo zimekuwa zikitekeleza Ujenzi wa madarasa 157 katika halmshauri nzima.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live