Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AKUTWA AMESHAKUFA BAADA YA KUZAMA BAHARINI

Bad News 10?fit=800%2C445 AKUTWA AMESHAKUFA BAADA YA KUZAMA BAHARINI

Sat, 29 Aug 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Abdulla Ali Mwadini mwenye umri wa miaka 47 Mkaazi wa Jambiani Kichakanyuki amekutikana akiwa amefariki dunia baada ya kuzama baharini wakati akiwa katika shughuli zake za uvuvi wa kuzamia huko Jambiani Kibigija Mkoa wa Kusini Unguja.

Kwa Mujibu wa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kusini Unguja Suleiman Hassan Suleiman amesema tukio hilo limetokea tare he 28-08-2020 majira ya 12:00 Asubuhi.

Nae Sheha wa Shehia ya Jambiani Kibigija Ali Mtumwa Hassan amekiri kupokea simu kutoka kwa raia mwema kuhusiana marehemu huyo kuwa amekutikana amefariki dunia na kusema kuwa alipokwenda eneo la baharini umeletwa mwili huo katika boti iliyotoka eneo la tukio

“Ni mvuvi ambae anafanya shughuli zake za Uvuvi katika Bahari ya Jambiani Kibigija ameondoka na wenzake katika shughuli zao za uvuvi mnamo alfajir mapema waliona vifaa vyake vikielea katika baharini walipomtafuta  katika eneo hilo hawakumkuta na ndipo kilipotumwa chombo kumtafuta na kuona  mwili wake  ukiwa umefariki dunia na huku ukiwa na jaraha kichwani na mwilini”.

Aidha Sheha huyo amewataka wavuvi kuwa makini katika Bahari na pia wanapokwenda kuvua baharini wafatane zaidi wawili ili panapotokea tatizo iwe rahisi kusaidia katika baharini .

Mwili wa marehemu huyo umefanyiwa uchunguzi wa kidaktari na kukabidhiwa jamaa zake kwa mazishi.

Story na Rauhiya Mussa Shaaban 

Chanzo: zanzibar24.co.tz