Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AJALI YA MOROGORO: Vifo vyafikia 89

71497 Ajali+pic

Thu, 15 Aug 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Majeruhi saba kati 32 wa ajali ya lori la mafuta ya petroli iliyoanguka na kulipuka mkoani Morogoro waliokuwa wakitibiwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), Dar es Salaam nchini Tanzania wamefariki dunia.

Hii ina maana kuwa waliofariki kutokana na ajali hiyo iliyotokea Jumamosi iliyopita ya Agosti 10, 2019 eneo la Msamvu mkoani Morogoro hadi kufikia saa 5.30 asubuhi  ya leo Alhamisi Agosti 15,2019 ni 89.

Akitoa taarifa hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano (MNH), Aminiel Aligaesha amesema kwa sasa wamebaki majeruhi 25 kati ya 46 waliopokelewa hospitalini hapo kutoka Hospitali ya Rufaa ya Morogoro.

Amesema kati ya majeruhi hao 16 wapo katika chumba cha uangalizi maalum (ICU) huku wengine tisa wakiendelea kupatiwa matibabu katika wodi maalum iliyotengwa kwa ajili ya majeruhi hao.

Aligaesha amesema madaktari wanaendelea kufanya jitihada kubwa kuokoa maisha ya majeruhi waliobaki.

“Madaktari na wauguzi wanafanya kila jitihada kwa weledi kuhakikisha majeruhi wanapatiwa matibabu kunusuru maisha yao,” alisema

Habari zinazohusiana na hii

Jana Jumatano, Agosti 14,2019, Mkuu wa Mkoa wa Morogoro, Stephen Kebwe akizungumza na waandishi wa habari alisema majeruhi waliolazwa mkoani humo ni 16 na wanaendelea vizuri.

Tayari miili zaidi ya 60 imezikwa katika makaburi ya Kola mkoani Morogoro ambapo miili yote imechukuliwa vipimo vya vinasaba (DNA) na  ndugu ambaye anafikiria katika ajali hiyo waliofariki ni ndugu zao anaweza kufika hospitalini kupimwa na kufananishwa kama vinafanana.

 

 

Endelea kufuatilia Mwananchi kwa taarifa zaidi.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz