Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

AFARIKI DUNIA BAADA YA KUZAMA BAHARINI

Drownhand616 AFARIKI DUNIA BAADA YA KUZAMA BAHARINI

Tue, 11 Aug 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Mtu mmoja anaetambulika kwa jina la Asaa Salim Ngwali anaekadiriwa kuwa na umri wa miaka 24 hadi 26 Mkaazi wa Kikwajuni Bondeni amefariki dunia baada ya kuzama baharini wakati walipokuwa akivua na wenzake katika chombo chao cha Mwakinyo huko Kizingo. 

Akizungumza na Zanzibar24  Sheha wa shehia ya Kikwajuni juu bi Asha Ali, amekiri kutokea kwa tukio hilo la kufariki kijana huyo na kuwataka wavuvi wa maeneo hayo kutoa taarifa kwa viongozi wa shehia ili kuweza kuwasaidia matatizo yao.

Ameongeza kusema kuwa mtu yoyote anaekwenda kwa ajili ya uvuvi au hata kuogelea kuwa makini ili kuweza kujiepusha athari zinazoweza kujitokeza.

Nae Mwenyekit wa Wavuvi wa jumuiya wa wavuvi Wilaya ya Mjini Salum Ndonga amesema kuwa ni kawaida Ya wakojani kuenda Baharini kwa ajili ya uvuvi na ndipo aliposhusha boya na kijana huyo kuingia katika maji na ndipo yalipomkuta mauti yake.

Aidha ndugu Salum  amewataka watu wenye matatizo ya kiafya kutokwenda kwenye shuhuli za uvuvi baharini. 

Story na Rauhiya Mussa Shaaban

Chanzo: zanzibar24.co.tz