Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT Wazalendo walalamikia figisu anwani za makazi

Anwani.crdownload Zoezi la anwani za makazi linaendelea nchi nzima

Tue, 26 Apr 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha ACT-Wazalendo kimemwandikia barua Mkuu wa Mkoa wa Kigoma, kikidai uwekaji wa majina ya mitaa na barabara unaoendelea, haufuati sheria na kanuni za majina ya barabara na mitaa.

Kimesema mchakato unaoendelea unakiuka misingi ya utawala bora na kwamba majina yanayowekwa siyo yaliyopitishwa na vikao halali na kukubaliwa na wananchi.

Mwenyekiti wa chama hicho Mkoa wa Kigoma, Sendwe Ibrahim, katika taarifa yake iliyotolewa jana, alisema wameshangazwa na uamuzi wa Wakala wa Barabara Vijiji (TARURA), kuwaamulia majina ingawa sio wenye mamlaka ya Mji wa Kigoma Ujiji.

“Itakumbukwa kuwa wawakilishi wa wananchi kupitia Baraza la Madiwani la Manispaa, waliamua kutoa majina ya mitaa kwa kuzingatia historia ya mji wetu kwa kuenzi watu maarufu wa mji wetu.

“Tumeshangaa sana kuwa baadhi ya mitaa imewekwa majina ambayo hayakupitishwa katika vikao vya juu kabisa vya mkoa kama RCC, mfano ni barabara ya kutoka Soko la Mwanga kwenda Uwanja wa Ndege wa Kigoma, ambayo iliamuliwa iitwe Dk. Amani Walid Kabourou,” alisema Ibrahim na kuongeza:

“Barabara ya kutoka Stesheni ya Reli kwenda Bangwe ambayo iliamuliwa kuitwa Che Guevara na Mtaa wenye Soko la Jioni ambao iliamualiwa kuitwa Mtaa wa Mzee Bakari Menge. Yote hii TARURA wamefuta kinyume na maamuzi ya vikao halali.”

Chanzo: www.tanzaniaweb.live