Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

ACT Wazalendo kuishtaki Serikali ya Tanzania ikizifunga laini za simu

ACT Wazalendo kuishtaki Serikali ya Tanzania ikizifunga laini za simu

Mon, 20 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Chama cha upinzani nchini Tanzania cha ACT Wazalendo kitafungua kesi mahakamani kupinga uamuzi wa Serikali wa kuzifunga laini za simu ambazo hazijasajiliwa kwa alama ya vidole.

Kabla ya kufungua kesi, uongozi wa chama hicho umeitaka Serikali ya Tanzania kusitisha mpango wa kufungia laini hizo na iwezeshe nyenzo za kutosha katika ofisi za Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (Nida). 

Kwa mujibu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), laini zote ambazo hazijasajiliwa kwa mfumo huo zitafungiwa huduma rasmi leo Jumatatu Januari 20, 2020 saa 5.59 usiku baada ya kufikia ukomo wa shughuli hiyo ya usajili lililoanza Mei mosi mwaka 2019.

"Kwa hiyo wasitishe na zoezi liendelee kwa sababu kulikuwa na uzembe mkubwa upande wao," amesema Ado Shaibu, Katibu wa Itikadi, Uenezi na Mawasiliano kwa Umma wa Chama hicho.

Shaibu ametoa kauli hiyo alipokuwa akizungumza na wanahabari leo Januari 20,2020 jijini Dar es salaam.

Kati ya Mei mosi mwaka 2019 hadi Januari 15, 2020, TCRA imesajili laini milioni 27.3, sawa na asilimia 56 ya laini milioni 48.7 tarajiwa.

Pia Soma

Advertisement

 "Vinginevyo wanasheria wetu watafungua kesi ndani ya siku saba zijazo kuanzia leo. Haiwezekani wananchi wakaadhibiwa kwa uzembe wa Nida," amesema Shaibu.

Amesema endapo Serikali ya Tanzania itakaidi, itafungua kesi kwa kutumia msingi wa kikatiba kupitia ibara ya 18, inayohusisha upatikanaji wa haki mbalimbali kwa watanzania.

"Tumebaini asilimilia 73 ya mkoa wa Kigoma hawajasajiliwa, tunaona kutakuwa na athari kubwa ikiwamo upotevu wa mapato kwa wananchi, hata serikalini, kwa hiyo tunashauri serikali isitishe mpango huo," amesema.

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz