Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

40 wanusurika, gari likigonga nyumba ya ofisa wa polisi

19106 Ajali+pic TanzaniaWeb

Tue, 25 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Abiria zaidi ya 40 wamenusurika kifo na wengine wanne kujeruhiwa, baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuacha njia na kuparamia nyumba ya ofisa mstaafu wa Jeshi la Polisi.

Ajali hiyo imetokea leo Septemba 24, 2018 eneo la Mabungo wilaya ya Moshi, mkoani Kilimanjaro katika barabara kuu ya Dar es Salaam - Moshi, baada ya basi la kampuni ya Capricon, kuacha njia na kuparamia nyumba hiyo.

Mashuhuda wa ajali hiyo wamedai basi hilo lilikuwa linajaribu kulikwepa gari dogo ndipo lilipoacha barabara na kuparamia nyumba ya ofisa huyo mstaafu aliyetambulika kwa jina la Abiudi.

Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Koka Moita amesema watu wanne wamejeruhiwa katika ajali hiyo na wamekimbizwa katika kituo cha afya kilichopo mji mdogo wa Himo.

"Taarifa kwamba wameumia kwa kiwango gani bado tunafuatilia ili tuwajuze zaidi, majeruhi wamekimbizwa kituo cha afya Faraja kilichopo Himo," amesema Kamanda Moita.

Mmiliki wa Kituo cha Afya Faraja kilichopo Himo, Samuel Minja, amesema kituo chake kimepokea majeruhi.

"Ni kweli kuna ajali na majeruhi wamepelekwa Faraja, lakini niko barabarani siwezi kutoa taarifa na kama ukiihitaji taarifa fika kituoni utaipata vizuri," amesema Minja.

Chanzo: mwananchi.co.tz