Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

3,056 wajitokeza migogoro ya ardhi, hati 1,474 zatolewa

John Kayombo.png 3,056 wajitokeza migogoro ya ardhi, hati 1,474 zatolewa

Wed, 25 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Jumla ya watu 3,056 waliokuwa na changamoto za ardhi katika jiji la Dodoma wamesikilizwa chini ya utaratibu wa kliniki ya ardhi uliofanyika kwa siku tano.

Wananchi hao walisikilizwa katika kliniki iliyoanza Oktoba 16 hadi 20, 2023 mkoani Dodoma.

Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, John Kayombo ameyasema hayo leo Jumanne Oktoba 24, 2023 katika taarifa yake aliyoitoa kwenye vyombo vya habari.

Kayombo amesema huduma zilizotolewa niutoaji wa hati miliki kwa haraka, kutoa elimu juu ya masuala ya ardhi, kurahisisha ulipaji wa kodi ya pango la ardhi.

Amesema hati 1474 zilitolewa papo hapo, maombi ya hati mpya 561 yalipokelewa, namba za malipo 1674 zilitolewa, viwanja 645 vilipandishwa katika mfumo, migogoro 774 ilisikilizwa, watu 149 walipata huduma za mipangop miji na watu 221 walipata huduma za upimaji.

Amezitaja changamoto walizokutana nazo kuwa ni upungufu wa vifaa ikiwemo kompyuta, watu kuwa wengi kwa siku moja na hivyo kufanya huduma kutolewa hadi usiku pamoja na upungufu wa watumishi hasa ikizingatiwa kuwa watumishi wa jiji waliosimamishwa.

“Changamoto nyingine ni eneo ambalo wamelifanyia kazi kuwa na kasi ndogo ya mtandao ILMIS (Mfumo wa Kutunza Kumbukumbu za Ardhi) na hivyo kufanya watoa huduma kuchukua muda kumhudumia mtu mmoja,” amesema.

Hata hivyo amesema kuwa hatua zilichukuliwa kukabiliana na changamoto hizo kwa kuwasiliana na wizara ambayo iliboresha upatikanaji wa mfumo wa ILMIS, kuongeza vitendea kazi hasa kompyuta na kuongeza idadi ya watumishi ili kuziba pengo la waliosimamishwa kazi.

Pia amesema kuhusu changamoto ya watu wengi waliojitokeza, wamepanga kuwahudumia kwa tarafa na kata ili kupunguza msongamano.

Kayombo amesema wamepanga zoezi hilo kufanyika kwa wiki moja kila mwezi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live