Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

2500 kuhitimu masomo yao Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino

85554216f97487a076007e91bf7d00b1 2500 kuhitimu masomo yao Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino

Thu, 28 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WAHITIMU 2500 wa Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino jijini hapa wanatarajiwa kuhitimu masomo yao katika ngazi tofautitofauti siku ya Ijumaa Januari 29 katika mahafali ya 22 ya Chuo hicho yatakayofanyika katika Uwanja wa Raila Odinga chuoni hapo.

Hayo yalisema na Makamu mkuu wa chuo hicho kampasi ya Mwanza,Profesa Costarick Mahalu.

Alisema kutakuwa na wahitimu 154 katika Shahada ya Uzamili(Masters) na wahitimu wawili ngazi ya Uzamivu(PHD) upande wa sheria. Alisema Wahitimu wengine watakuwa wa vitivo vya Elimu,Uhandisi na Sheria.

‘’Kila mwaka Tunajaribu kuleta wahitimu ambao elimu yao/Maarifa yameelekezwa zaidi katika kulisaidia Taifa.Lengo kubwa la wahitimu wetu tunawashauri wajijajiri wao wenyewe’’ alisema Profesa Mahalu.

Profesa Mahalu alisema ongezeko la wahitimu limeongezeka kutokana na vijana wengi kipindi hiki wamekuwa na sifa za kujiunga vyuo vikuu.

‘’Bado tunachangamoto sana vyuo vikuu vingi havina uwezo wa kujijenga kwakuwa wengi tumekuwa tukitegemea ada katika kujiendesha’’ alisema profesa Mahalu.

Alisema Chuo chao kimeanza kutekeleza agizo la Rais wa awamu ya Tano, Dk John Magufuli ya kufundisha masomo ya Jiografia na Historia.

Alisema Wameanza mipango ya kufundisha historia na Jiografia itakayoonyesha historia ya Mwafrika ikoje na jiografia yetu ikoje.

Alisema Rais Magufuli amekuwa akizungumzia muda mrefu sana kuwa uhuru wa kiuchumi unaanzia katika kujua historia ikoje na vijana wengi wa kitanzania hawajui historia.

Prof Mahalu alisema Rais Magufuli amehimiza sana masomo ya historia na Jiografia tuyape kipaumbele sana

Chanzo: habarileo.co.tz