Sat, 13 Jan 2024
Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Wachimbaji wadogo 16 wa madini ya dhahabu katika mgodi wa Ikinabushu uliopo kijiji cha Ikinabushu kata ya Gilya tarafa ya Dutwa wilayani Bariadi mkoani Simiyu wamepoteza maisha baada ya kufukiwa na kifusi huku miili mingine ukiendelea kuopolewa.
Taarifa zinaeleza kuwa tukio hilo limetokea alfajiri ya Januari 10, 2024 wakati wakiendelea na zoezi la uchumbaji ambapo mgodi huo una takribani siku tatu tangu uanze kazi ya uchumbaji.
Kwa mujibu wa wasimamizi wa mgodi huo wamesema awali shughuli za uchumbaji zilisitishwa lakini wachimbaji hao wakaingia kinyemela kuchimba
Chanzo: www.tanzaniaweb.live