Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto azungumzia kugombea urais 2020

90436 Zittob+pic Zitto azungumzia kugombea urais 2020

Tue, 31 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Zitto Kabwe amesema atakuwa tayari kugombea nafasi ya urais katika uchaguzi mkuu ujao mwaka 2020 endapo vyama watakavyoshirikiana navyo katika mchakato huo vitaridhia.

Zitto ametangaza msimamo leo Jumanne, Desemba 31,2019 wakati akitoa salamu za mwaka mpya za ACT- Wazalendo huku akiwapa pole  wananchi waliofikwa na changamoto mbalimbali katika kipindi cha mwaka 2019.

Amesema hivi sasa sio suala nani anafaa kugombea bali ni mchakato wa wadau na vyama vya siasa kukaa chini pamoja kuangalia namna ya kukiondoa chama tawala cha CCM.

Zitto amesema baada ya wadau na vyama vya siasa kukaa pamoja  kinachofuata ni kuangalia kuwa kutokana na changamoto zilizopo fulani anafaa kugombea kiti cha urais.

"Suala siyo mimi kugombea  bali ni mazingira  na muktadha. Kwa wenzangu wakisema kulingana na mazingira haya Zitto anafaa kugombea sitokimbia msalaba huu,” amesema Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini

Alipoulizwa kuhusu kutogombea ubunge iwapo atagombea urais, Zitto amesema, "suala la hapa sio  nauweka ubunge wangu rehani hapana. Unapokuwa kwenye mapambano lazima uwe tayari kwa lolote."

Chanzo: mwananchi.co.tz