Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto azungumzia akaunti zake kudukuliwa, Nape na Bashe nao walonga

64664 Zittto+pic.png

Thu, 27 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kiongozi wa chama cha upinzani Tanzania cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amewataka wananchi mbalimbali ndani na nje ya Tanzania kupuuza  taarifa zozote zinazoenezwa kupitia akaunti zake za kijamii.

Zitto amesema akaunti zake za Twitter, Facebook na Instagram zimedukuliwa na watu aliodai wamehusika kumteka mfanyabiashara mwenye asili ya Kenya, Raphael Ongangi ndio wanatumia akaunti hizo. Hata hivyo, polisi wamezungumzia suala tukio hilo.

Mwanasiasa huyo amesema mara ya mwisho kutumia akaunti zake ilikuwa Juni 11, 2019 baada ya kukamatwa na kuwekwa kizuizini na Idara la Uhamiaji Zanzibar ambao walimzuia kusafiri kwenda Kenya.

Mara baada ya kumwachia, Zitto  hakupewa  simu yake ya mkononi na kompyuta mpakato ‘laptop.’

Amesema amewasiliana na wamiliki wa mitandao hao ambao tayari wamezisimamisha huku akisema, “naomba pole sana kwa usumbufu wowote utakaokuwa umejitokeza.”

Mapema leo Alhamisi Juni 27, 2019, akaunti hizo hususan  ya Twitter zilituma jumbe mbalimbali zikizungumzia hali ya kisiasa na mitizamo yake ‘Zitto’ kwa utawala wa Rais wa Tanzania, John Magufuli.

Pia Soma

Ujumbe wa kwanza kutumwa ilikuwa saa 5.48 asubuhi uliosema, “Ni kweli tumekuwa tukiikosoa Serikali kwa muda mrefu lakini lazima nikiri kuwa kuna mabadiliko makubwa yamefanywa na serikali hii ya JPM. Japokuwa ninajua kuna baadhi ya viongozi aliowateua wanamuangusha kiuhalisia MAGUFULI amefanya mengi.”

Ujumbe mwingine ulikuwa, “Nilisema tangu mwanzo sitashiriki siasa za kupinga maendeleo yanayofanywa na serikali hii ya @MagufuliJP na sasa nimeamua kwa moyo wa dhati kabisa ninaamua kuunga mkono kwani ni kwa maendeleo ya wote. Kiongozi mbinafsi kwa vyovyote hawezi kuona haya yanayofanyika kwa sasa.”

Saa 7.26 mchana, akaunti hiyo ilituma ujumbe mwingine ukisema, “Nawakaribisha pia @HusseinBashe na @Nnauye_Nape ambao wameshachukua kadi za uanachama ACT Wazalendo na wanaosubiri ni kuvunjwa tu kwa #Bunge na bila kumsahau mdogo wangu @JMakamba. Hakika ACT Wazalendo itaitikisa Chadema ambayo inatamba kuwa Chama Kikuu cha Upinzani.”

Hussein Bashe ambaye ni Mbunge wa Nzega Mjini (CCM) aliuchukua ujumbe huo na kuuweka kwenye akaunti yake ya Twitter kisha akaandika, “Wanaofahamu siasa za Tanzania na za vyama na wanaonifahamu vizuri misimamo ama maamuzi yangu ya kisiasa huwa sifanyi kwa njia za kificho ama za kichimvi, Siku nikiamua kuondoka CCM nitaondoka hadharani, sitasubiri njia za kificho ama za kichimvi kama hizi mnazo OTA.”

Hakuishia hapo, aliandika tena, “Hili Genge la kihuni ambalo linaongozwa na wahuni wachache ipo siku nitawataja kwa majina ila mpango wenu wakutaka kunifanya nione CCM si chama sahihi kwa mimi kuwatumikia wananchi wa Nzega na Tanzania HAUTAFANIKIWA, CCM bado nipo sanaaaaaa, shindaneni na mm kwa hoja na si vioja.”

Naye Nape ambaye ni Mbunge wa Mtama (CCM) ameandika ujumbe kwenye akaunti yake ya Twitter akiambatanisha picha akiwa yeye, Zitto pamoja na January Makamba ambaye ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira)

Ujumbe huo unasema, “Nimeona tweets zinazodaiwa kuwa za Ndg Zitto zikinitaja. {Kakanusha sio zake}. Kilichonishangaza ni uwezo mdogo wa kufikiri wa wadukuaji! Mnanyimwa usingizi na nini?? Hamuwezi kuendelea na maisha MSIPONITAJA!! Khaaaa!”

 

Kauli ya Polisi

Kamanda wa Polisi mkoa wa Kipolisi Mkoa wa Kinondoni limesema askari polisi wamesambazwa mtaani ili kufuatilia mtu aliyemteka Raphael.

Kamanda wa mkoa huo, Musa Taibu amesema tulipokea taarifa kutoka kwa mke wake Veronika Kundya akidai mmewe Rafael wakiwa kwenye gari lao walikingwa na gari mbele yao na kumchukua mume wake huku wakimueleza ana mazungumzo naye

Wakati watu hao wakizungumza na Rafael hakuweza kusikia maneno yaliyokuwa yakizungumzwa kwa kuwa walimuingiza kwenye gari lingine.

“Bahati mbaya hakujua namba ya gari na aina ya gari kwa bahati mbaya jeshi la polisi hatuna vithibitisho hivyo, tunaendelea na uchunguzi kama ni kweli ametekwa na tuna imani tutafanikiwa kwa kuwa tumewasambaza askari polisi mtaani ili kufuatilia,” alisema Taibu.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Chama cha ACT Wazalendo kimesema akaunti ya mtandao wa twita inayomilikiwa na Kiongozi wa chama hicho, Zitto Kabwe imedukuliwa na wahalifu wa mitandaoni na sasa inatumika bila matakwa yake baada ya kupata neno siri inayotumika kufungulia ukurasa wake.

Katika taarifa aliyoisambaza leo Alhamisi Juni 27, 2019, kupitia mitandao ya kijamii, Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa chama hicho Ado Shaibu amesema simu na kinakilishi(Laptop) yake bado vinashikiliwa na Jeshi la Polisi.

“Taarifa zinazowekwa hivi  sasa kwenye akaunti ya Twitter ya  Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Ndugu Zitto Kabwe si zake. Simu na laptop ya Ndugu Zitto vipo mikononi mwa Jeshi la Polisi.

Baada ya kudukuliwa kwa akaunti hiyo, leo katika ukurasa wa Zitto kuna na ujumbe tofauti na utamaduni wake alioujenga wa kuikosoa serikali kwa mara, na moja ya ujumbe unasema:

 

Chanzo: mwananchi.co.tz