Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto awaangukia wananchi Kigoma

Zitto Pic Zitto awaangukia wananchi Kigoma

Mon, 5 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amewaangukia wananchi na wanasiasa wa mkoa Kigoma akiomba radhi kwa mabaya yeyote aliyowafanyia wakati wa mchakato wa harakati za kisiasa na kuwaomba waungane pamoja kuelekea uchaguzi Mkuu wa mwak 2025.

Kabwe alisema hayo katika uwanja wa barafu kwenye mji mdogo wa Mwandiga alipokuwa akimtambulisha aliyewahi kuwa mbunge wa viti maalum CUF, Kiiza Mayeye ambaye amejiunga na ACT Wazalendo.

Kiongozi huyo wa ACT Wazalendo ambaye amewahi kuwa mbunge kwa miaka 15 kwenye majimbo mawili tofauti mkoani Kigoma alisema kuwa wakati wa harakati za kisiasa mambo mengi yanatokea ambayo wakati mwingine yanawakwaza watu ingawa inaweza kuwa bila kukusudia hivyo akachukua nafasi hiyo kuomba radhi na kuomba asamehe kwa yote yaliyotokea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live