Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto asema wapinzani kukimbilia CCM ni vita ya kisaikolojia

11930 Pic+zitto TanzaniaWeb

Tue, 14 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe ametoa ushauri kwa viongozi wenzake wa vyama vya upinzani kujiandaa kwa ajili ya kushiriki katika chaguzi nyingine zote zinazofuata.

Amewataka kujitathmini wakati wa kuelekea chaguzi ndogo zijazo, uchaguzi wa serikali za Mitaa mwaka ujao na Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Zitto ambaye ni Mbunge wa Kigoma Mjini amebaini kwamba wanasiasa wa upinzani wakiwamo wabunge na madiwani kukimbilia CCM kwa sababu yoyote ile ni vita ya Kisaikolojia inayolenga kuwakatisha tamaa wanachama wa vyama vya upinzani, wafuasi na wananchi.

Ameandika wasikubali kuingizwa katika vita hiyo.

Zitto ametoa kauli hiyo leo Agosti 14 kupitia ukurasa wake wa Twita.

CCM imeshinda katika kata zote pamoja na jimbo hilo kupitia mgombea wake, Christopher Chiza.

“Baada ya kugomea chaguzi za Songea Mjini na Singinda Kaskazini, ni dhahiri hatupaswi kugomea chaguzi nyingine yeyote. Ushirikiano madhubuti wa vyama vya upinzani (kimkakati) na wapenzi wa demokrasia unahitajika zaidi wakati huu kuliko wakati mwingine wowote. Kwa mfano kuwe na watazamaji wa ndani kwa kila chaguzi ili waweze kukusanya kila taarifa za ukiukwaji wa sheria au kanuni za uchaguzi,”ameandika Zitto.

Katika ufafanuzi wa hoja yake, Zitto amesema miezi michache ijayo mashambulizi dhidi ya vyama vya upinzani na wanaharakati wa haki za binadamu na haki za demokrasia yataongezeka zaidi.

“Wale tu wenye dhamira ya dhati ya kujenga Tanzania yenye Maendeleo ndani ya Demokrasia ndiyo watabaki na tutashinda hatimaye.”ameandika.

 

Chanzo: mwananchi.co.tz