Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto asema mwaka 2021 ulikuwa na mitihani mikubwa

ZITTO KABWE Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Fri, 31 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa Chama Cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema mwaka 2021 ulikuwa wenye mitihani mikubwa huku akiweka wazi mambo watakayofanya kwa mwaka 2022.

Zitto amesema hayo leo Desemba 31,2021 katika salamu zake za kuhitimisha mwaka 2021 na kuukaribisha mwaka mpya 2022.

Bila kuitaja mitihani hiyo, Zitto amesema “Mwaka 2021 ulikuwa mwaka wenye mitihani mikubwa. Tunamshukuru Mwenyezi Mungu kuvuka mitihani hiyo.”

Amebainisha mipango ya chama hicho kwa mwaka ujao, akisema kuwa wanatarajia uwe mwaka wa maridhiano ya kitaifa ya kupata Tume Huru ya Uchaguzi na katiba mpya.

“Mwaka 2022 kitaifa tunataraji utakuwa mwaka wa Maridhiano ya Kitaifa yatakayofanikisha kupata Tume Huru ya Uchaguzi itakayofanikisha kupata Katiba Mpya inayokubalika na wote kama Taifa” amesema Zitto nakuongeza

“Tutatumia kila nafasi kufikia kila mtu au taasisi itakayowezesha kupata Maridhiano ya Kitaifa”

Advertisement Amesema wanatarajia kufanya mageuzi ambayo watayatangaza kwenye mkutano mkuu utakaofanyika mwishoni mwa mwezi Januari.

“Tutaanza kufanya kazi ya kuisimamia Serikali Nje ya Bunge kwa kuundwa kwa Kamati ya Kuisimamia Serikali ambayo itatazama kila Wizara ya Serikali na kutumia Sera na Ilani yetu ya Mwaka 2020 kupendekeza Sera Mbadala” amebainisha Zitto

Ametaja mpango mwingine kuwa ni kujenga upinzania madhubuti kwa kuimarisha chama kuanzia ngazi ya mitaa.

“Tutatumia mwaka 2022 kuimarisha Chama katika Vijiji, Mitaa, Kata na Majimbo iii kujenga upinzani madhubuti wenye kuzingatia masuala ya watu.” amesema

Pia ameeleza kuwa chama hicho kitazindua mfumo wa kidijitali wa kusaidia wanachama wa cha ahicho kuibua masuala mbalimbali

“Tutazindua #ACTkiganjani: Mfumo wa kigitali wa kusajili wanachama na kuwawezesha wanachama kuibua masuala mbalimbali kwenye maeneo yao iii yafanyiwe kazi na viongozi wa juu. Tutawaweka karibu wanachama iii kusaidiana kiuchumi na kijamii. Nawatakia mwaka mpya 2022 wenye mafanikio, faraja na mshikamano” amesema Zitto

Chanzo: www.tanzaniaweb.live