Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto arejea nchini, asema hana hofu

96199 Pic+zito Zitto arejea nchini, asema hana hofu

Tue, 18 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo nchini Tanzania, Zitto Kabwe amerejea nchini baada ya kumaliza ziara yake katika mataifa mbalimbali ikiwemo Marekani na Uingereza.

Zitto ambaye pia ni mbunge wa Kigoma Mjini (ACT- Wazalendo) amerejea jana Jumatatu Februari 17,  2020 ambapo amesema ziara yake nje ya nchi ilikuwa na mafanikio makubwa.

Akizungumza baada ya kuwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) amedai kuwa pamoja na kupewa vitisho lakini bado hana hofu ndio mana maana amerudi nchini

“Sina hofu na ndio maana nimerudi bila shida yoyote kwa sababu hamna kosa lolote nimefanyana nimetekeleza wajibu wangu kama kiongozi wa kisiasa kama mbunge na sina hofu kabisa, nitaendeea kufanya shughuli zangu kawaida,.” amesema

 

Akielezea ziara yake, Zitto amesema ziara hiyo ilikuwa na mafanikio makubwa

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement

 

“Ziara ilikuwa na mafanikio makubwa sana na ndio maana watawala wanahangaika na kuendelea na vitisho kwa sababu ya mafanikio ya ziara niliyokuwa nayo,."amesema Zitto bila kusema watawala wanahangaika na nini

 

Zitto ambaye pia ni mwanzilishi wa chama hicho amesema kuwa kwa sasa chama chake kiko kwenye mchakato wa uchaguzi na anatafakatri kuwa anachukua fomu ya kugombea nafasi gani ndani ya chama hicho

“Kuna mchakato wa uchaguzi ndani ya chama, kuna taratibu za kuchukua fomu na bado natafakari nichukue fomu ya nafasi gani ya chama, na kesho (leo) tunaweza kufanya utaratibu wa kuchukua fomu na kuendelea na utaratibu mwingine” amesema kiongozi mwasisi huyo wa ACT- Wazalendo

Zitto, akiwa nchini Marekani, alianza kushukiwa na wabunge katika mkutano wa 18 wa Bunge uliomalizika hivi karibuni mjini Dodoma kwa kitendo chake cha kuiandikia barua Benki ya Dunia (WB) akitaka isiidhinishe mkopo wa Sh1.2 trilioni kwa Tanzania kwa ajili ya sekta ya elimu.

Jambo hilo lililaaniwa na wabunge wa CCM, huku Spika Job Ndugai akisema watamsubiri arejee nchini ili wamuulize sababu za kufanya hivyo, na hapohapo akamtaka Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuangalia kama kuna uwezekano wa kuwemo jinai katika kitendo hicho.

Chanzo: mwananchi.co.tz