Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto ampongeza Rais Samia kwa Amani na utulivu

Zito Pichhhhhjmj Zitto ampongeza Rais Samia kwa Amani na utulivu

Tue, 18 Oct 2022 Chanzo: mwanachidigital

Kiongozi wa chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema hali ya kisiasa nchini imekuwa ya utulivu na kwamba hali hiyo ya utulivu inasaidia kuchochea shughuli za maendeleo.

Akizungumza leo Oktoba 18, 2022 wakati akitoa salamu zake kwa Rais Samia, Zitto amesema njia ya kujenga maridhiano ya kitaifa ndio njia pekee itakayoifanya nchi isonge mbele.

Zitto amesema makala aliyoandika Rais Samia Suluhu Hassan ya Julai 1 siku ya kuadhimisha miaka 30 ya mfumo wa vyama vingi alielezea falsafa yake ya R4 kwaajili ya kuliweka taifa pamoja na kulijenga,hivyo aanamuomba Rais aweze kuendeleza hizo za mageuzi ya kisiasa.

“Nachukua nafasi hii kukupongeza Rais Samia kwa juhudi za kuwaweka Watanzania pamoja bila kujali itikadi zao.

“Uwepo wangu hapa ni ishara kuwa haiangalii vyama vya siasa vya watu bali unawaangalia watanzania kwa pamoja,” amesema Zitto Kabwe.

Zitto amesema Rais Samia anaweza kujenga miundombinu yakiwemo madaraja, barabara, viwanja vya ndege na bandari, lakini Watanzania watamkumbuka kwa mawazo aliyoyaanisha katika Makala yake hiyo yenye dhamira ya kuwaleta Watanzania pamoja.

Adiha amesema chama chake wanatarajia kuwasilisha uchambuzi na mapendezo yao kuhusiana na muswada uliowasilishwa bungeni wa Bima ya Afya kwa Wote, hivyo ameomba Serikali yake ipokee mawazo yao na kuyafanyia kazi.

“Sisi kama chama cha upinzani tumefanya uchambuzi wetu na tutawasilisha mapendekezo yao ya kuboresha muswada huo, tunaomba Serikali yako ipokee na itafakari ushauri wetu,” amesema.

Chanzo: mwanachidigital