Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto amnadi mgombea wa Chadema Buyungu

10058 Pic+zitto TanzaniaWeb

Sat, 4 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe amewataka wananchi wa Kata ya Kasuga wilayani Kakonko mkoani Kigoma kumchagua mgombea ambae atakuwa na uwezo wa kuisukuma serikali kuboresha maendeleo kwa wananchi.

Zitto alitoa kauli hiyo juzi wakati akimnadi mgombea ubunge kwa tiketi ya Chadema, Elia Kanjero katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kijiji cha Kasuga.

Alisema vyama vya upinzani vina dhamira ya kuwatumikia wananchi katika kuchochea maendeleo yao, hivyo wananchi wanatakiwa kumchagua Kanjero akisema ni kiongozi ambaye atakuwa dira kwa wananchi katika suala la maendeleo na nchi kwa ujumla.

‘’Wananchi hamtakiwi kubabaishwa na jambo lolote, hapa tulipo kila mtu anaujua ukweli. Mfano kwa jimbo hili hakuna la kuwaficha maana nyinyi ni wenyeji na viongozi wenu mnawajua kuanzia wabunge waliokuwapo na waliyoyafanya mliyashuhudia na madhaifu mnayajua, iweje mshinikizwe kuongozwa na mtu wakati mnajua ukweli?

“Mpeni kura za kutosha huyu kijana Elia awatumikie,” alisema Kabwe.

Mgombea huyo anashinda na wagombea wengine wanane, akiwa wa CCM, Christopher Chiza aliyewahi kuwa mbunge wa jimbo hilo.

Meneja wa kampeni za Chadema Buyungu, Alfonce Mbasa aliwataka wananchi kuhakikisha wanashiriki uchaguzi huo utakaofanyika Agosti 12, mwaka huu bila kuogopa vitisho vinavyotolewa na baadhi ya watu.

Alisema zipo mamlaka ambazo ni kazi yake kuhakikisha wanalindwa kwa kuwa ni haki ya kila mwananchi aliyejiandikisha na mwenye umri wa miaka 18 kupiga kura.

Akizungumza na wananchi, Mgombea Kanjero aliahidi kushirikiana na wananchi hao katika kuchochea maendeleo ya jimbo ili kukuza uchumi wa wananchi.

Chanzo: mwananchi.co.tz