Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto aeleza Tanzania itakavyokuwa ACT- Wazalendo ikishinda 2020

90487 Zittob+pic Zitto aeleza Tanzania itakavyokuwa ACT- Wazalendo ikishinda 2020

Tue, 31 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kiongozi wa ACT- Wazalendo nchini Tanzania, Zitto Kabwe amesema endapo chama hicho kikishika dola katika uchaguzi wa mwakani kitahakikisha kinaijenga Tanzania inayopaa kiuchumi kwa kubuni na kutekeleza sera za uchumi shirikishi utakaozalisha ajira.

Pia, Zitto ambaye ni mbunge wa Kigoma Mjini amesema ACT-Wazalendo itahakikisha inavutia uwekezaji wa nje ili kuongeza mitaji nchini na kupanua shuguli za uzalishaji mali.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Desemba 31, 2019 wakati akitoa salamu za chama hicho kuhusu mapokezi ya mwaka mpya wa 2020 ambao utakuwa na uchaguzi mkuu.

"Ni muhimu wananchi kufahamu tutapokea uongozi wa nchi wenye changamoto lukuki zinazotokana na muundo wetu na idadi ya watu. Najua changamoto hizi nyingine zinatokana na chama kilichopo madarakani," amesema

Zitto amesema watahakikisha wanaongeza idadi ya watalii nchini hadi kufikia milioni sita kwa mwaka ili kutengeneza ajira zitakazoongeza fedha za kigeni sambamba kuweka sera bora zitakazojenga uwezo wa kila mtu kufaidika na rasirimali zilizopo.

Amefafanua ACT- Wazalendo inawaza Tanzania yenye huduma nzuri za kijamii kwa kutoa bora itakayoenda na wakati na kuzalisha wahitimu wenye uweledi, ubunifu na uwezo wa kushindana  katika soko la ajira.

"Lengo letu kuwa na huduma bora na nafuu za afya zitakazowakinga na kuwatibu wananchi kwa kuwa na zahanati na vituo vya afya vya kutosha. Pia, tutahakikisha kunakuwa na huduma ya uhakika ya majisafi na salama," amesema Zitto.

Mbali na hilo, Zitto amesema chama hicho, kitajenga mfumo imara wa utoaji haki kwa kujenga uwezo wa kupambana  na rushwa , kuondoa vikwazo vilivyosababishwa watu kuonewa katika kipindi cha miaka minne.

"Hii ndio ndoto ya ACT- Wazalendo na ndio maoni ya wananchi tuliokutana nao kupitia ziara yetu ya listening tour. Tanzania yenye maisha ya raha na furaha yaani kazi na bata," amesema Zitto.

Akizungumzia mwaka 2019, Zitto amesema ulikuwa mgumu wa Watanzania, vyama vya upinzani na alijikuta akihudhuria mahakamani karibu nusu mwaka kwa ajili ya kesi na kuangalia marafiki zake wakiwamo wa vyama upinzani.

Chanzo: mwananchi.co.tz