Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto abeba kero za wananchi ugumu maisha, ajira za vijana

Zitto Kabwe Drt Zitto abeba kero za wananchi ugumu maisha, ajira za vijana

Mon, 12 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha ACT- Wazalendo, kimehitimisha ziara yake ya awamu ya pili, huku kikisema changamoto zaidi ya tano zimeibuka katika mikutano ya hadhara waliofanya katika mikoa 11 ukiwamo Shinyanga.

Kimesema miongoni mwa changamoto hizo ni ugumu wa maisha, kikokotoo, ajira kwa vijana, afya bora kwa wananchi, Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini (Tasaf), tatizo la Wamachinga na migogoro ya wakulima na wafugaji.

Ziara hiyo ni awamu ya pili iliyohitimishwa leo Jumapili Juni 11, 2023 katika Uwanja wa Furahisha jijini hapa ilikuwa na lengo la kutambulisha dira ya ACT- Wazalendo ya ‘Ahadi Yetu kwa Watanzania’ na dhamira ya kujenga ‘Taifa la Wote kwa Maslahi ya Wote’.

Dira hiyo ilizinduliwa Februari 18 mwaka huu, ikiwa na lengo la kuweka mkazo kwenye maeneo ya sera za uchumi, ustawi wa jamii na afya ya jamii.

Pia dira hiyo iliyozinduliwa na viongozi wakuu wa ACT- Wazalendo wakiongozwa na Zitto Kabwe imejikita katika kuhakikisha kila Mtanzania ananufaika na rasilimali zilizopo na kila mtu aishi kwa heshima.

Waziri Kivuli wa Fedha na Mipango, Immanuel Mvula amesema changamoto zimejitokeza katika mikoa ya Ruvuma, Rukwa, Shinyanga, Geita, Njombe, Mara, Simiyu na Mwanza ambako wanahitimisha ziara yao ya mikutano ya hadhara na kujiimarisha.

"Haya ni mambo yanayowaumiza wananchi katika mikoa 11 tuliopita na viongozi wenzangu wakuu katika ujenzi wa chama na kusikiliza kero za wakazi wa maeneo husika," amesema Mvula akihutubia.

Hata hivyo, hivi karibuni Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdallah Ulega ameliambia Mwananchi kuwa Serikali kupitia bajeti ya mwaka 2023/24 na CCM wana mipango mizuri ya kukabiliana na changamoto hiyo.

Wakati Mchinjita akieleza hayo, makamu mwenyekiti wa ACT- Wazalendo (bara), amesema katika ziara hiyo wamekutana na malalamiko ya baadhi ya wastaafu wakilia na kanuni mpya za kikokotoo.

"Tunataka Serikali irudishe kikokotoo cha mwaka 2017 na kuachana na hiki kipya kinachompunja mafao mstafuu ambapo mafao ya mkupuo yameshuka kutoka asilimia 50 hadi 33. Pia miaka ya kumlipa mstaafu imeshuka kutoka 15 hadi 12.5 kwa kikokotoo cha sasa," amesema Semu.

Semu ametoa wito kwa vyama vya wafanyakazi kuungana na kutetetea maslahi ya wafanyakazi huku akitaka kuboreshwa kwa menejimenti ya mifuko ya hifadhi ya jamii sambamba na Serikali kulipa madeni inayodaiwa na mifuko.

Mei 16 mwaka 2022 Serikali ilitangaza kanuni hizo mpya ikisema itakuwa na manufaa mengi ikiwemo mifuko ya pesheni ya PSSSF na NSSF itaimarika na kuwa endelevu kwa kuongeza kiwango cha malipo ya mkupuo kutoka asilimia 25 iliyokataliwa mwaka 2018 hadi asilimia 33.

Kwa mujibu wa Serikali kanuni hiyo mpya itakuwa na vikokotoo kikiwemo cha mkupuo kitakuwa na asilimia 33 kwa mifuko yote, kikotoo limbikizi kitakuwa 1/580. Pia mshahara wa kukokotoa mafao ya pensheni utakuwa wa mishahara bora ya miaka mitatu ndani ya miaka 10 kabla ya kustaafu na umri wa kustafuu.

Kuhusu suala la wamachinga, Zitto amesema sio vema wamamchinga kuondolewa katikakati ya miji na kupelekwa katika maeneo yasiyo rafiki na shughuli zao.

"Ni lazima tuangaike na suala la matumizi ya miji iwe kwa wamachinga sio kwa watu wenye uwezo pekee.Nimeambiwa hapa jijini Mwanza wameondolewa na kupelekwa huko dampo ambako hakuna shughuli.

"Leo hii Makoroboi imegeuka kuwa maegesho ya magari baada ya kuondolewa wamachinga siyo sahihi, Serikali inapaswa kuiga mfano wa manispaa ya Ujiji (Kigoma) ya kutenga mitaa kwa ajili ya Wamachinga. Tunawaomba wananchi wa Mwanza tupeni Halmashauri za Ilemela na Nyamagana ili muone mabadiliko," amesema Zitto.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live