Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto: Uchaguzi 2024 unaweza kusimamiwa na chombo ambacho hakipo Kisheria

Zitto Pic Mwanasiasa wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe

Wed, 1 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwanasiasa wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe amesema Sheria mpya ya Tume ya Uchaguzi imefuta Sheria zote za Uchaguzi za zamani na hivyo TAMISEMI imefutwa rasmi kusimamia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa

Amesema “Sheria ya Uchaguzi bado haijatungwa, hivyo kuna uwezekano mkubwa wa Uchaguzi wa 2024 kusimamiwa na Chombo ambacho hakipo katika Sheria. Hilo ni jambo ambalo Waandishi wanatakiwa kuwa nalo makini na kulifuatilia kujua kwanini Sheria haijatungwa mpaka sasa.”

Ameongeza kuwa changamoto katika chaguzi ikiwemo suala la uwepo wa Kura Bandia bado lipo akidai hivi karibuni Mkoani Kigoma, Vijana wa ACT-Wazalendo walikamatwa na kufikishwa Mahakamani licha ya kuwa wao ndio walioripoti uwepo wa Kura Bandia

Chanzo: www.tanzaniaweb.live