Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto: Ripoti Kikosi Kazi haijakidhi matakwa yetu

Zitto 4?fit=680%2C453&ssl=1 Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo nchini

Fri, 28 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe amesema ripoti ya kikosi kazi cha kuratibu maoni ya wadau kuhusu demokrasia ya vyama vingi, haina mambo waliyoyataka kwa asilimia 100, lakini ni hatua moja mbele.

Zitto amebainisha hayo leo Oktoba 28, 2022 wakati wa mkutano wa viongozi wa dini na wanasiasa kujadili na kuchambua ripoti ya kikosi kazi iliyokabidhiwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan.

Amesema kwenye mijadala yoyote, mtu hawezi kupata kila kitu ambacho anakitaka, bali atapata machache na mengine atayakosa.

Amewataka Watanzania kupokea kidogo walichokipata na kuendelea kupigani yale waliyoyakosa.

"Ripoti hii siyo asilimia 100 ya kile ambacho watu wangependa kiwe, lakini ni hatua moja mbele. Kuna baadhi ya mambo tumefanikiwa na baadhi ya mambo hatukufanikiwa," amesema Zitto ambaye alikuwa mjumbe wa kikosi kazi.

Akizungumzia mambo ambayo hawakufanikiwa, Zitto ametaja lile la wakurugenzi wa halmashauri kutumiwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (Nec) kama wasimamizi wa uchaguzi.

Lingine amesema ni uchaguzi wa serikali za mitaa kusimamiwa na Tume ya Uchaguzi, akisema jambo hilo liliibua mvutano wakaamua kuliacha kama lilivyo huku wakutaka tafiti zaidi zifanyike.

Kuhusu mambo ambayo wamefanikiwa, Zitto amesema ni suala la ruzuku kwa vyama vya vidogo vya siasa pamoja na kupunguza mamlaka ya Msajili wa Vyama vya Siasa ili afanye kazi kama Msajili na siyo kama mdhibiti wa vyama vya siasa.

"Rai yangu kwa Watanzania ni kwamba tuitumie ripoti hii katika kuongeza hamasa ya kufanya mabadiliko ya mambo ambayo tunayataka," amesema Zitto kwenye mkutano huo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live