Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto: Kikosi kazi kitakwamua mchakato wa Katiba

Zitto (600 X 337) Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa chama cha ACT-Wazalendo nchini

Thu, 27 Oct 2022 Chanzo: mwanachidigital

Siku tano baada ya Rais Smia Suluhu Hassan kupokea mapendekezo ya ripoti ya kikosi cha kuratibu na kuchakata maoni ya wadau wa demokrasia Kiongozi wa Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amesema, kikosi kazi kimetoa mapendekezo ya kukwamua mchakato wa Katiba.

Zitto ameyasema hayo leo Jumatano Otoba 26 katika mjadala uliohusu Ripoti ya Kikosi Kazi kupitia mtandao wa ‘Twitter space’ ulioandaliwa na Mwananchi Communications Ltd.

Amesema walipendekeza mambo mbalimbali yakukwamua mchakato wa katiba yaliyoikwamisha mwaka 2014 ikiwemo aina ya Muungano, idadi ya serikali na mambo ambayo yanahusu Tawala za mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi).

“Hatua ya kwanza lazima kuwe na mkutano wa kitaifa kuangalia ni mambo gani yalikwamisha mchakato mwaka 2014 na hatua ya pili ni kupeleka muswada wa mabadiliko ya sheria bungeni,” amesema Zitto.

Amesema ili kufikia mkwamo huo, ni lazima kuuhisha sheria ya mabadiliko ya katiba, ukishakubali mchakato uwe vipi unapopelekwa bungeni kunakuwa hakuna shida kwa kuwa kila mtu atakuwa anazungumza lugha moja.

“Hatua ya tatu ni kuundwa kwa jopo la wataalamu kuangalia rasimu ya Jaji Warioba, na mkutano wa kitaifa uwe marejeo na baada ya kupata rasimu ya katiba iende bungeni moja kwa moja,” amesema.

Chanzo: mwanachidigital