Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto Kabwe kuhusu kauli ya Jaji Mutungi kuzuia mikutano ya kisiasa

Kabwe2 Zitto Kabwe, Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo.

Tue, 7 Sep 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, ameupongeza uamuzi wa Msajili wa Vyama nchini, Jaji Francis Mutungi, wa kuwakutanisha kwa pamoja viongozi wa vyama vya siasa na Jeshi la Polisi kwa ajili ya kujadili tofauti zao zilizopo ili kusafisha taswira ya nchi.

Kiongozi huyo amesisitiza haya kupitia Mtandao wa kijamii wa Twitter na kusema kuwa mkutano huo haupaswi kwani vyama vinapaswa kufanya kazi zao za kisiasa kwa uhuru zaidi na kudai kuwa Jeshi la Polisi limekuwa likivunja sheria na kuzuia Vyama kufanya kazi zao.

"Uamuzi wa Msajili wa Vyama vya Siasa, kuitisha Kikao kati ya Mkuu wa Jeshi la Polisi na Vyama vya siasa ni Uamuzi sahihi. Polisi wamekuwa wanavunja Sheria hovyo na kuzuia Vyama kufanya kazi zao za kisheria. Mkutano huo usichelewe Vyama vifanye kazi zao za kisiasa kwa Uhuru" Amesema kiongozi huyo wa ACT-Wazalendo.

Hata hivyo, Msajili wa Vyama vya siasa, amesema kuwa tayari ameshafanya mawasiliano na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, Kamanda Simon Sirro, kwa ajili ya kujadili mvutano huo uliopo baina ya pande hizo mbili.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live