Mwanasiasa mkongwe kutoka Chama cha ACT Wazalendo Zitto Kabwe amemtaka Waziri wa Nishati na uchukuzi Makame Mbarawa kujiuzulu akidai kuwa amewadanganya wabunge na amesisitiza kuwa kabla ya kujiuzulu anapaswa kuwaomba radhi wabunge kutokana na uongo wake.
Zitto ameongeza kuwa mtu mwingine anayepaswa kujiuzulu ni mkurugenzi mkuu wa TANROADS ambaye amemtaka kujiuzulu haraka iwezekanavyo ama Rais amfukuze kazi mara moja kutokana na kushidwa kutimiza majukumu yake ipasavyo.
Zitto ameishauri Serikali kuona kama kuna haja ya kuunganisha Wizara ya ujenzi na Wizara ya uchukuzi kwani kupitia muunganiko wake mambo mengi yamekwama kama reli ya kisasa, upanuzi bandari, Viwanja vya ndege pamoja na ujenzi wa Barabara.