Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto Kabwe: Nautaka Urais

Zitto Wa Urais Zitto Kabwe

Sat, 7 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiongozi wa Chama cha ACT- Wazalendo Zitto Kabwe ameweka bayana kuwa anatamani kuwa Rais wa Jmahuri ya Muungano wa Tanzania siku moja kwani anaamini anao uwezo wa kuwatumikia wananchi kutokana na uzoefu alionao katika siasa lakini pia maarifa.

“Nimesema siku zote kwamba urasi nautaka, siwezi kusema moja kwa moja kwamba nitagombea mwaka 2025, kwasababu uamuzi huo unatokana na kwanza kudra za mungu na pia Chma na wananchi ambao ndiyo lazima watoe ridhaa na dhamana ya kuiongoza nchi katika nafasi hiyo,” alisema Zitto

Kiongozi huyo amegusia suala la kuitoa madarakani CCM kuwa siyo jambo rahisi na ili kukamilisha lengo hilo Vyama Vya Upinzania havina budi ya kuungana na kusimamisha mgombea mmoja amabaye ataweza kupambana kuhakikisha CCM inatoka madarakani.

Zitto pamoja na viongozi wengine wa Chama cha ACT- Wazalendo wameweka kambi ya zaidi ya mwezi mmoja mkoani Mwanza ambako wanafanya kampeni ya kuimarisha chama.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live