Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto: Hatutaacha kupigania haki

Zitto Kabwe ACT Leader3 Zitto: Hatutaacha kupigania haki

Mon, 13 Mar 2023 Chanzo: mwanachidigital

Kiongozi wa chama cha ACT- Wazalendo, Zitto Kabwe amesema chama hicho hakitakata tamaa na kitaendelea kupigania haki za wananchi ikiwemo kuchagua viongozi wanaowataka kuwaongoza.

Mbali na hilo, Zitto amesema watahakikisha wanaendelea kusemea pia changamoto zinazowakabili wananchi ili kuhakikisha zinapatiwa ufumbuzi na kutoa mawazo mbadala kwa Serikali kupitia baraza kivuli la chama hicho.

Ametoa kauli hiyo, jana Jumapili Machi 12, 2023 wakati akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika uwanja wa Baraza la Eid wilayani Tunduru mkoani Ruvuma. Mkutano huo ni mwendelezo wa ziara ya kuimarisha chama hicho, iliyowahusisha viongozi wakuu.

Zitto amesema ndio maana ya uchaguzi mkuu mwaka 2020 kumalizika na CCM kunyakua viti vya udiwani na ubunge, ACT- Wazalendo kiliendelea kusema changamoto mbalimbali za Watanzania pamoja na kudai demokrasia mazingira ya siasa kuwa mazuri.

" Ndio maana tuliamua kuunda baraza la mawaziri kivuli ili kusemea changamoto za wananchi na kutoa mawazo mbadala kwa Serikali.

"Tulikuwa na machaguo tuendeleea na mapambano au tupambane ndani ya nchi, lakini tukasema hatuwezi kukimbiia changamoto zilizojitokeza.

Zitto ambaye ni mbunge wa zamani wa Kigoma Kaskazini, amesema baada ya kumalizika kwa uchaguzi mkuu 2020 alifuatwa na balozi tatu zilizompa ofa ya kuondoka kutoka mazingira kutokuwa rafiki baada ya mchakato huo kumalizika.

"Lakini nikawaambia siwezi kuondoka...Sisemi hivi kudogosha waliokimbia nje ya bali katika mapambano kuna njia nyingi za kukabiliana na tatizo," amesema Zitto.

Katibu Mkuu wa ACT- Wazalendo, Ado Shaibu amewataka wananchi Tunduru kuendeleza mshikamano na mapambano, licha ya kutochaguliwa kuwa mbunge wa Kaskazini atahakikisha anabeba hoja na ajenda zinazowakabili wananchi wa majimbo ya Tunduru Kaskizini na Kusini.

Katika mkutano huo, Shaibu pia aligusia suala la uvamizi wa tembo katika makazi ya watu, akiitaka Serikali kufanya utafiti wa kubaini sababu za wanyama hao kutoka mbugani kwenda katika vijiji na kuleta madhara kwa wananchi wanaoishi maeneo hayo.

Waziri Kivuli wa Kilimo, Abdallah Mtutura wa ACT- Wazalendo, alisema suala la wakulima kujiorodhesha kwa ajili ya kupata mbolea sio mzuri, akisema unawaletea usumbufu mkubwa kwa wananchi hasa wakulima wa maeneo yenye uzalishaji mkubwa wa mazao.

Chanzo: mwanachidigital