Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Zitto, Bwege na viongozi 6 waachiwa kwa dhamana

ZITTO HURU Zitto, Bwege na viongozi 6 waachiwa kwa dhamana

Thu, 25 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wapo pia viongozi 6 waliokamatwa jana... Watakiwa kurejea kituo hapo Julai Mosi mwaka huu.... Kiongozi Mkuu wa Chama cha ACT-Wazalendo, Zitto Kabwe, Mbunge wa Kilwa Kusini, Suleiman Bungara na viongozi wengine 6 wa chama hicho wameachiwa kwa dhamana na kutakiwa kurejea kituo hapo Julai 1 mwaka huu wakituhumiwa kwa kosa la kuhatarisha amani.

Akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi baada ya kuachiwa na Polisi Zitto amesema kuwa hapo awali wakiwa kituo cha polisi wilayani Kilwa walishitakiwa kwa kosa la kuandamana bila kibali cha polisi lakini walipofikishwa kituo cha Polisi Wilaya ya Lindi mashitaka yao yalibadilishwa na kuwa ni kuhatarisha amani.

"Leo asubuhi tumechukuliwa finger print (alama za vidole) ,tumepigwa picha kama wahalifu na baada ya mzunguko mrefu tukapewa taarifa kwamba kosa letu limebadilika na kuwa kuhatarisha amani " amesema Zitto

Zitto na wenzake walikamatwa jana wilayani Kilwa wakiwa katika mkutano wa ndani wa chama hicho katika ziara ya kiongozi huyo ya kupokea wanachama mbalimbali waliohamia katika chama hicho hivi karibuni.

Zitto alikuwa katika ziara yake ya kichama ya kupokea viongozi na wanachama kutoka vyamavingine waliohamia katika chama hicho hivi karibuni na mpaka anakamatwa ilikuwa ni siku ya pili tu ya ziara yake hiyo katika Mikoa ya Kanda ya Kusini akianzia wilayani Rufiji katika Mkoa wa Pwani.

Katika ziara zake hizo ,Zitto Kabwe amekuwa akisisitiza madai ya tume huru ya uchaguzi jambo ambalo limekuwa likipigiwa kelele za viongozi wa vyama vya upinzani pamoja na asasi mbalimbali za kirai nchini lakini akashauri vyama makini vya upinzani kutokususia uchaguzi huo licha ya kutokuwepo kile alichoita tume huru ya uchaguzi katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live